7

Siku mbili zilizopita, kakaetu wa Bongo Mr. blue aka kabyser ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya kuachia vibao Mapozi, Pesa, Baki na Mimi alijipatia jiko lake rasmi. Dada kwa jina Waheeda ndie alieukonga moyo wa mtanashati huyu naye akaamua kumpa heshma yake kama wajibu unavyodai. Wapenzi hawa wamekuwa wakiishi pamoja kwa mda sasa na wana watoto wawili warembo. Waheeda aliwahi kuwa video vixen na ni travel agent.

Mr. Blue aliwahi kumdate mwimbaji Naj ambaye hivi sasa anatoka kimapenzi na Baraka da Prince na wanadaiwa kupata mtoto pamoja.

Tunamtakia kila la kheri katika ndoa yake na huu ni mfano bora kwa wasanii wenza ambao wengi wameshindwa kumudu jukumu la ndoa na wameishia kutumbukia katika anasa.

.blue-32

6

Post a Comment

 
Top